Mlipuko wa Ebola ambao umesababisha vifo vya takriban watu 131 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huenda ukaenea kwa kasi zaidi kuliko ilivyodhaniwa awali, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameonya.
Dkt Anne Ancia aliiambia BBC kwamba kadiri shirika hilo linavyochunguza ndivyo inavyodhihirika kuwa maambukizi yameenea katika maeneo mengine.
Maafisa walisema zaidi ya watu 513 wanashukiwa kuambukizwa nchini DR Congo kufikia Jumanne, huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki katika nchi jirani ya Uganda.
Utafiti wa Kituo cha MRC chenye makao yake mjini London cha Uchambuzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Ulimwenguni uliotolewa Jumatatu ulipendekeza kulikuwa na “ugunduzi mkubwa” wa chini, na kwamba haiwezi kudhibiti kuwa tayari kulikuwa na kesi zaidi ya 1,000.
Utafiti huo ulipendekeza kuwa mlipuko wa sasa ni “mkubwa kuliko ilivyothibitishwa sasa” na kwamba “uhalisia wa ukubwa wake bado haujabainika”.
Shirika la Msalaba Mwekundu lilionya kwamba Ebola inaweza kusambaa haraka ikiwa walioambukizwa hawatatambuliwa mapema, kwa sababu jamii hazina habari na mifumo ya afya imezidiwa, na kuongeza kuwa “tunashuhudia haya yote” katika mlipuko wa sasa.
Siku ya Jumatatu Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi alitoa wito wa “utulivu” na kuwataka raia wa Congo kuwa makini na kuzingatia ushauri wa wahudumu wa afya, baada ya kufanya mkutano wa dharura na maafisa wake Jumatatu jioni.
Mkuu WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye alitangaza mlipuko huo kuwa janga la kimataifa wiki iliyopita, alisema “ana hofia sana na ukubwa na kasi ya janga hilo”.
Taarifa ya BBC