Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesafiri kuelekea nchini Rwanda kuhudhuria mkutano wa Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika.
Samia ataungana na Wakuu wa Nchi na Serikali kwenye mkutano huo utakaoandaliwa leo Jumanne, Mei 19, 2026 jijini Kigali.
Mkutano huo wa kimataifa unawakutanisha wataalamu wa nishati, wawekezaji na mashirika ya kimataifa, ambapo utajadili matumizi ya nishati ya nyuklia kwa maendeleo ya Bara la Afrika.
Mkutano huo pia unalenga kujadili njia bora ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme Afrika, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kusaidia maendeleo ya viwanda, kukuza ubunifu wa teknolojia za nishati ya nyuklia pamoja na kuvutia wawekezaji katika miradi ya nishati.