Rachel Wandeto mwanamke aliyesifika mitandaoni kwa kujichora picha ya Rais William Ruto, katika mwili wake ameripotiwa kufariki mapema Jumatatu.
Wandeto ambaye ni mkazi wa Mwiki, alilazwa Hospitali kuu ya Kenyatta, mwishoni mwa wiki jana baada ya kuchomwa na watu wasiojulikana.
Yamkini marehemu alipata majeraha ya moto ya asilimia 70, baada ya kuteketezwa na wanaume watatu wasiojulikana.
Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, alimtembelea Wandeto hospitalini Jumapili jioni huku akilaani shambulizi hilo.
Polisi wameanzisha msako wa waliohusika kwa mauaji hayo.