Watu wawili wameripotiwa kuaga dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea eneo la Guangxi, nchini Uchina, siku ya Jumatatu.
Tetemeko hilo la kiwango 5.2, katika vipimo vya richa limewalazimu zaidi ya watu 7,000, kutoroka makwao katika mji wa Liuzhou .
Nyumba 13 ziliporomoka katika mkasa huo wa mapema Jumatatu ambao ulisambaratisha usafiri.
Hata hivyo reli,na laini za mawasiliano hazikuathiriwa kutokana na tetemeko hilo .