Mkondo wa pili wa mashindano ya mbio za magari ya Shell AutoX Rally, yataandaliwa Jumapili hii Mei 17, katika eneo la Stoni Athi, kaunti ya Machakos.
Baadhi ya madereva waliotoa ithibati kushiriki ni mama na bintiye Tinashe Gatimu na Caroline Gatimu,Neel Gohil,Suleiman Munyua na Michuki Hinga.
Kampuni ya Uchina ya Kove, inawakilishwa kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo pamoja na JCB na Royal Enfield Kenya.
Makala ya mwaka huu yanatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa kufuatia ushindani mkali ulioshuhudiwa mwaka jana.