Waziri wa Afya wa Uingereza Wes Streeting ajiuzulu

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa afya wa Uingereza Wes Streeting amejiuzulu.

Huku Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akikabiliwa na shinikizo la kujiuzulu, serikali yake inazidi kupata pigo za kisiasa, la  hivi karibuni likiwa kujiuzulu kwa Waziri wa Afya Wes Streeting.

Streeting amesema amechukua hatua hiyo kwa kuwa hana imani na uongozi wa Waziri Mkuu Starmer, akiongeza kuwa  Starmer hatakiongoza chama cha Labour kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Starmer anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu, huku akikabiliwa na changamoto kuu la uongozi hasaa baada ya chama cha labour kupoteza viti 1,100 katika uchaguzi wa manispaa.

Hata hivyo, Starmer ameahidi kukabiliana na changamoto kuu zinazokabili taifa hilo, akiwaonya mawaziri wake kuwa mabadiliko ya uongozi yatalitumbukiza taifa hilo katika vurugu.

Share This Article