Wabunge wastahimili mvua wakila kiapo Uganda

Wabunge wanaokula viapo vya kuhudumu katika bunge hilo wanajumuisha 529, kutoka chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).

Dismas Otuke
1 Min Read

Wabunge wamestahimili mvua kubwa mapema Alhamisi, katika siku ya pili kula viapo vya kuhudumu katika bunge la 12 nchini Uganda.

Hafla hiyo ilianza Jumatano siku moja baada ya kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni kwa muhula wa saba afisini.

Wabunge wanaokula viapo vya kuhudumu katika bunge hilo wanajumuisha 529, kutoka chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).

Wabunge hao waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Januari mwaka huu, wanatarajiwa kuhudumu afisini hadi mwaka 2031.

Share This Article