Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmwe anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu huku zaidi ya wabunge 70 wakiunga mkono aondoke mamlakanai.
Shinikizo hilo limetokana na matokeo mabaya katika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Uingereza, huku shinikizo kubwa la kumtaka aondoke wadhifani likitoka ndani ya chama chake.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shabana Mahmood, ambaye pia ni mwanachama wa Baraza la Mawaziri, yumo miongoni mwa wanaomwomba Starmer ajiuzulu.
Mbunge wa Labour, Jonathan Hinder, ambaye pia alitoa wito wa kujiuzulu kwake, alisema: “Hakuna waziri mkuu anayeweza kuendelea hivi. Ni wakati wa kuwa wakweli, anaondoka.”
Tarehe 11 Mei, Waziri Mkuu Starmer alitoa hotuba iliyolenga kupunguza shinikizo la kisiasa lililokuwa likiongezeka, akisisitiza kuwa hatajiuzulu.
Alikiri kuwa serikali imefanya makosa, lakini akasisitiza kuwa imechukua “maamuzi sahihi makubwa ya kisiasa”.
“Ninajua wapo wanaonitilia shaka, na najua lazima nizithibitishe hizo shaka kuwa si sahihi, na nitafanya hivyo,” alisema akijaribu kutoa ujumbe wa utulivu.
Starmer pia aliahidi kurejesha uhusiano wa karibu na Ulaya.
Taarifa ya BBC