Wanachama wa ODM wanaotaka kuwania nyadhifa watakiwa kutuma maombi

Tom Mathinji
1 Min Read
Kiongozi wa chama cha ODM Oburu Oginga.

Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), kimewataka wanachama wake wanaolenga kuwania nyadhifa mbali mbali kutuma maombi, huku chama hicho kikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.

Nyadhifa hizo ni pamoja na Urais, Gavana, Seneta, Mwakilishi Mwanamke, Mbunge na Mwakilishi Wadi.

Kamati ya Kitaifa ya Ushirikishi wa Uchaguzi (NECC), imetangaza kuwa wale watakaotuma maombi hayo, ni sharti wawe wanachama wa ODM ambao wanatimiza sheria za uteuzi za chama hizo.

Watakaowasilisha maombi hayo wamehimizwa kufanya hivyo kupitia tovuti ya chama hicho kufikia Juni 30, 2026.

“Ili kufanikisha mchakato wa kuaminika, tunawahimiza wanachama kuwasiliana na kamati ya NECC, kwa maelezo zaidi,”  alisema mwenyekiti wa NECC Emily Awita.

Share This Article