Kundi la mwisho la wanariadha wa Kenya laekea Ghana

Kenya iliyo na kikosi cha wanariadha 74 itashiriki katika mbio  na mashindano ya ndani ya uwanja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kundi la pili na la mwisho la wanariadha wa Kenya, limeondoka nchini Jumapili kuelekea Accra,Ghana, kushiriki makala ya 24, ya mashindano ya Riadha Barani Afrika.

Wanariadha wapatao 35 na maafisa liliondoka kujiunga na kundi la kwanza lililoondoka nchini siku ya Jumamosi.

Mashindano hayo yataandaliwa kati ya Mei 12 na 17, huku Kenya ikilenga kuboresha matokeo ya mwaka 2024 mjini Doula,Cameroon ilikomaliza ya pili.

Kenya iliyo na kikosi cha wanariadha 74 itashiriki katika mbio  na mashindano ya ndani ya uwanja.

Share This Article