Kenya na Ufaransa zimetia sahihi mikataba ya ushirikiano katika sekta mbalimbali kwenye mkutano ulioandaliwa Jumapili jioni katika Ikulu ya Nairobi.
Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo, Rais William Ruto wa Kenya alikariri kuwa Kenya, itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Ufaransa katika sekta mbalimbi kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Mikataba iliyosainiwa ni katika sekta ya uchimbaji madini,sekta ya fedha,usafiri wa reli na kawi.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Marcon pia amesema wataendelea kuinga mkono mikataba ambayo imekuwepo na kuongeza ushirikiano katika nyanja mbalimbali.
Rais Macron yuko nchini kwa ziara rasmi ambapo anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la Afrika, litakaloandaliwa katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano KICC.
Kongamano hilo litakalowashirkisha zaidi ya Marais 30, litafanyika Jumatatu na Jumanne wiki hii.