Wizara ya Afya ya Lebanon imesema kuwa mashambulizi ya Israeli ya 24 yameua watu 51, wakiwemo wahudumu wawili wa afya.
Katika taarifa, Wizara hiyo ilisema kwamba Adui Israeli anaendelea kukiuka sheria za kimataifa na misingi ya kibinadamu, akiongeza uhalifu zaidi dhidi ya wahudumu wa afya.
Kwa mujibu wa Wizara, mashambulizi hayo yalilenga moja vituo viwili vya Mamlaka ya Afya huko Qalawiya na Tibnin, wilaya ya Bint Jbeil, katika mashambulizi mawili ya angani.
Makubaliano ya kusitisha mapigano, yaliyosimamiwa na Marekani, sasa yanaingia wiki yake ya tatu.
Wizara hiyo ilisema watu 2,846 wameuawa kote nchini Lebanon tangu Machi 2, wakati majeshi ya Israeli yalianzisha operesheni mpya ya kijeshi.
Tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa unasema angalau wahudumu wa afya 103 wa Lebanon wameuawa na wengine 230 kujeruhiwa katika zaidi ya mashambulizi 130 ya Israeli.
“Tuko chini ya tishio kila sekunde, kila siku,” alisema Ali Safiuddin, mkuu wa Idara ya Ulinzi wa Raia ya Lebanon mjini Tyre kusini mwa Lebanon.
Safiuddin aliongeza kusema kwamba wanaishi kwa hofu ya kutojua iwapo watapona au watauawa na kwamba wamepoteza watu wengi sana na ni kana kwamba wao pia tayari wamekwisha.
Sheria za kimataifa za kibinadamu zinaelekeza kwamba wahudumu wa afya na wale wa kwanza kutoa msaada lazima walindwe wakati wa migogoro ya silaha lakini hali inaonekana kuwa tofauti katika matukio haya.