Rais Macron alakiwa Ikulu ya Nairobi, na Rais Ruto

Macron yuko nchini kuongoza kongamano la Africa Forward, litakaloandaliwa katika chuo kikuu cha Nairobi baina ya Mei 11 na 12.

Dismas Otuke
0 Min Read

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amelakiwa katika Ikulu ya Nairobi, na mwenyeji wake Rais William Ruto Jumapili jioni.

Macron yuko nchini kuongoza kongamano la Africa Forward, litakaloandaliwa katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano KICC, baina ya Mei 11 na 12.

Ruto na Macron wanatarajiwa kufanya majadiliano yanayolenga kuimarisha ushirikiano wa Kenya na Ufaransa.

Zaidi ya Marais 30, wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo .

Share This Article