Amos Kiprotich na Doreen Kibet washinda mbio za Iten Betika

Denis Kipkurui, alimaliza wa pili kwa dakika 44 na sekunde 47, akifuatwa na Kiprono Kipkemoi, aliyehitimisha tatu bora kwa muda wa dakika 44 na 59 seconds.

Dismas Otuke
2 Min Read

Amos Kiprotich na Doreen Kibet, ndio washindi wa makala ya mwaka huu ya mbio za kilomita 15 za Betika zilizoandaliwa mjini Iten siku ya Jumapili.

Mbio hizo zilizokuwa na washiriki 1,000, zilizushuhudia Amos Kiprotich, aliye na umri wa miaka 25, akitwaa ushindi kwa wanaume baada ya kuzitimka kwa dakika 44 na sekunde 33.

Denis Kipkurui, alimaliza wa pili kwa dakika 44 na sekunde 47, akifuatwa na Kiprono Kipkemoi, aliyehitimisha tatu bora kwa muda wa dakika 44 na 59 seconds.

Kiprotich amesema kufanya mazoezi Iten, kumemsaidia pakubwa kunoa makali yake kwa mbio za leo.

“Nilikuwa natarajia ushindani mkali leo kutoka kwa wapinzani wangu na nimezitumia kujiandaa kwa mashindano mengine makubwa yajao.”akasema Kiprotich

Doreen Kibet aliye na umri wa miaka 23 kutoka Kapsabet, ameshinda mbio za wanawake akiziparakasa kwa dakika 51 na sekunde 6.

Judy Jepnge’tich na Naomi Chemweno walimaliza katika nafasi za pili na tatu kwa dakika 52 na dakika 52 na sekunde 10 mtawalia.

Mkurugenzi wa kampuni ya Betika Eric Mwiti alisema”Iten imekuwa kigezo cha kuwakuza wanariadha.Kuwaona wanariadha zaidi ya 1,000 kujisajii kwa mbio za leo ina maana kuwa mbio za Betika Iten, zinazidi kukuwa na kupata umaarufu .”

Kiprotich na Kibet wametuzwa shilingi robo milioni kila mmoja huku waliomaliza katika nafasi za pili wakiondoka na shilingi 150,000, na laki moja kwa waliochukua nafasi za tatu.

Share This Article