Samuel Muchina kupeperusha bendera ya UDA kwenye uchaguzi mdogo wa Ol Kalou

Tom Mathinji
1 Min Read

Samuel Muchina Nyagah atapeperusha bendera ya chama cha UDA, kwenye uchaguzi mdogo wa Ol Kalou baada ya kuibuka mshindi katika Uchaguzi wa mchujo wa chama hicho kwa kupata kura 3,221.

Alifuatwa kwa karibu na George Wambugu Kanuri, almaarufu Delight, aliyepata kura 3,077,  Peter Njoroge Mugo akiwa wa tatu kwa kupata kura 1,049.

Uteuzi huo uliwavutia wawaniaji 10, licha ya kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo, ambapo wapiga kura 8,000 wakijitokeza ikilinganishwa na wapiga kura 72,000 waliosajiliwa katika eneo hilo.

Kwenye hotuba yake ya kukubali ushindi huo,  Nyagah alitaja uteuzi huo kuwa uliotekelezwa kwa njia huru na uwazi, akitoa wito kwa wawaniaji wenzake kuungana na kufanya kazi pamoja kuhakikisha UDA inapata ushindi kwenye Uchaguzi mdogo utakaoandaliwa Julia 16, 2026.

Wengine waliowania kwenye uteuzi huo ni pamoja na Peter Njoroge Mugo (1049), Mary Nyokabi Kamau (406), Peter Chuchu Njuguna (158), Maina Kiambati (96), Joseph Ndirangu (90), Ezekiah Kamweru (66), Daniel Ndungu (52) na Stanley Mwangi (43).

TAGGED:
Share This Article