Rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae afariki akiwa na miaka 86

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 86, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais aliye mamlakani Duma Boko ametangaza  kifo cha Mogae, ambaye alikuwa madarakani kati ya mwaka 1998 na mwaka 2008 ,kabla ya kustaafu.

Mogae aliyekuwa Rais wa tatu nchini Botswana, amefariki mapema Ijumaa na anakumbukwa kwa kuwa mstari wa mbele kuongoza vita dhidi ya virusi vya HIV, alipokuwa mamlakani.

Marehemu Mogae alihudumu katika nyadhfa mbalimbali serikalini ikiwemo waziri wa Fedha na baadaye Makamu wa Rais, kabla ya kuchaguliwa Rais.

Share This Article