Kenya iko ange dhidi ya Hantavirus

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Kenya imeweka uchunguzi mkali katika bandari ya Mombasa, na pia uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA, ili kukabiliana na visa vyovyote vya Hantavirus.

Ingawa wizara ya afya imesema kuwa ugonjwa huo sio tishio nchini Kenya,imeweka vituo vya kuchunguza kwa wageni wote wanaoingia.

Aidha, uchunguzi maradufu unafanywa katika vituo vya meli kutia nanga katika kaunti ya Mombasa, baada ya visa vya kwanza vya ugonjwa huo kuripotiwa kwa wasafiri wa meli katika bahari ya Atlantic.

Abiria watatu waliokuwa kwenye meli iliyosafiria kwenye  bahari ya Atlantic ,waliripotiwa kuaga dunia mapema mwezi huu kutokana na virusi hivyo.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya ulimwenguni (WHO), Thedos Ghebreyesus, alisema jana Alhamisi kuwa wagonjwa wengine watatu wanatibiwa baada ya kugunduliwa na ugonjwa huo.

Share This Article