Chama cha Kenya United Generation Party (KUG), ndicho cha hivi punde kusajiliwa tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Akikabidhi cheti mapema Jumatano, Msajili wa vyama vya kisiasa nchini John Lorionokou ,ametoa changamoto kwa chama hicho kudumisha demokrasia na maazimio yake kwa Wakenya.
“Mnaingia katika mazingira magumu na ni lazima mjitume kupigania nafasi yenu ili kuonekana. Mojawapo wa majukumu ya vyama vya kisiasa nchini ni kukumbatia na kudumisha demokrasia ya nchi .”akasema Lorionokou
Katibu Mkuu wa KUG,Dkt.Vincent Munyoki, amesema lengo lao ni kuwasilisha wagombezi katika viti vyote kuanzia kwa Rais hadi mwakilishi wadi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
“Sisi kama KUG tutasimamisha wagombeaji katika viti vyote hadi Rais, katika uchaguzi wa mwaka ujao,”akasema Dkt Munyoki

Munyoki ametoa changamoto kwa vijana kuwa katika mstari wa mbele kutwaa nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, akisisitiza kuwa wanalenga kumaliza ukabila na ubaguzi ambavyo vimekuwa mwiba kwa ugavi wa raslimali nchini.
KUG ni chama ambacho kimetengezwa na kuundwa na vijana wa hii nchi,tunasema kuwa Kenya, sio ya mtu au kabila moja ni yetu sisi sote.Akaongeza Dkt Munyoki
Chama hicho cha kisiasa ambacho ni cha 94, kusajiliwa nchini kina kaulimbiu ya “Tuko Rada,Tuko Macho.