Mary Muthoni achaguliwa mwenyekiti wa Makatibu wa Wizara ya Afya Afrika

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni.

Katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni, amechaguliwa mwenyekiti wa Makatibu wa Afya barani Afrika kwenye mkutano ulioandaliwa Jijini Brazzaville, nchini Congo.

Uchaguzi huo ni hatua kubwa katika kuimarisha ushirikishi wa hatua za utekelezaji afya ya umma na kupiga jeki jukumu la Kenya kuhakikisha maswala ya afya yanapewa kipaumbele barani Afrika.

Uteuzi huo wa Muthoni aidha, unatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kuboresha utambuzi wa magonjwa, kukabiliana na hali za dharura na kupanua uvumbuzi na mbinu bora Afrika.

Wakati huo huo, hatua hiyo pia itachochea ushirikiano na utekelezaji wa mifumo ya kiafya inayolinda jamii na kuunga mkono ajenda ya kuhakikisha huduma bora za afya kwa wote.

Wadhifa huo unaashiria kujitolesa kwa pamoja kwa mataifa ya Afrika kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za kiafya kupitia uongozi wa pamoja na ushirikiano wa kimkakati.

TAGGED:
Share This Article