Wafanyakazi wa umma nchini Botswana, walipewa mapumziko ya nusu siku Jumatatu kusherehekea ushindi wa timu ya mita 400 kwa wanariadha wanne wanaume kupokezana kijiti siku ya Jumapili.
Timu hiyo iliyomjumuisha bingwa wa Olimpiki Letsile Tebogo, ilishinda dhahabu na kuweka rekodi mya ya dakika 2 sekunde 54.47 .
Wafanyakazi wa umma nchini Botswana, walifunga kazi saa sita na dakika 45 Adhuhuri, ili kujumuika na wenzao kwa shamrashamra hizo za ushindi.
Mapumziko hayo yalitangazwa na Mkurugenzi wa huduma za serikali punde baada ya kumalizika kwa mbio za Dunia za kupokezana kijiti Jumapili jioni mjini Gaborone,Botswana.