Nyota wa zamani wa Chelsea Drogba atua Tanzania

Aliwasili jana, akifafanua kwamba alialikwa na Waziri wa Michezo Paul Makonda lakini hakutoa maelezo zaidi

Marion Bosire
1 Min Read

Nyota wa zamani wa timu ya soka ya Chelsea na timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast Didier Drogba yuko nchini Tanzania kwa ziara.

Drogba aliyewasili nchini humo jana, alifafanua kwamba alialikwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda lakini hakutoa maelezo zaidi.

Alionekana kwenye picha na video hiyo jana akifanya mazungumzo na Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambapo alisema kwamba anafurahia kurejea Tanzania na anatizamia kukutana na watu wa taifa hilo.

Mchezaji huyo wa zamani wa soka ya kulipwa ambaye jina lake halisi ni Didier Yves Drogba Tébily alistaafu rasmi kutoka uchezaji huo mwaka 2018.

Tangu wakati huo amekuwa akijihusisha na usaidizi wa wasiobahatika katika jamii kupitia wakfu wake unaoangazia afya na elimu barani Afrika.

Kando na hilo, anahusika pia na usimamizi wa soka ambapo yeye ni Naibu Rais wa shirika la kimataifa la amani na michezo na aliwahi kuwania Urais wa shirikisho la Soka la Ivory Coast.

Waziri Makonda bado hajasema lolote kuhusu ujio wa Drogba lakini anatarajiwa kufanya hivyo wakati wowote kutoka sasa.

Share This Article