Kenya,Japan zaimarisha ubia

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri mwenye Mamlaka Musalia Mudavadi, amekariri kujitolea kwa Kenya kuimarisha ushirikiano wake na Japan .

Akizungumza jijini Nairobi katika afisi yake alipokutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Japan, Toshimitsu Motegi,Mudavadi, alitaja ushirikiano wa Japan na Kenya, kuwa nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi Kenya.

Mudavadi alisema mazungumzo yao yalijikita katika ushirikiano katika sekta za biashara,uekezaji,maendeleo na ushirikiano wa Kidiplomasia.

Kenya na Japan zimekuwa na ushirikiano wa zaidi ya miongo sita katika sekta za Kilimo,Kawi,afya,Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,miundombinu,elimu na utalii.

Mataifa hayo mawili yalikiri kuwepo kwa tofauti kubwa ya kibiashara kati yao na kuhimiza haja ya kupunguza pengo hilo.

Share This Article