Idadi ya watoto wanaozaliwa na kulelewa na Mama pekee bila uwepo wa Baba mzazi iliongeza kwa asilimia 14.7 mwaka 2025, ikilinganishwa na mwaka 2024.
Kulingana na shirika la kitaifa la takwimu (KNBS), jumla ya watoto 168,158, wasiokuwa na baba walizaliwa mwaka uliopita ikilinganishwa na 148,657, waliozaliwa mwaka 2024.
Watoto waliozaliwa na akina mama walio katika ndoa walichangia asilimia 85 ,ya watoto wote waliozaliwa mwaka jana.
Jumla ya Watoto 1,144,847 ,walizaliwa mwaka jana kulingana na takwimu za KNBS.
Kati ya idadi hiyo watoto wa kiume waliozaliwa walikuwa asilimia 51.4, dhidi ya asilimia 48.6 ya wasichana.
Watoto huntha 17 walizaliwa mwaka jana, ikiwa ongezeko kutoka kwa 9, waliozaliwa mwaka 2024.