Yanga kuzuru chaka la Simba leo derby ya Kariakoo

Dismas Otuke
1 Min Read

Kivumbi kinatarajiwa leo Jumapili jioni wakati Simba watawaalika mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu Tanzania bara ,Young Africans ukipenda Yanga, katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, kisiwani Zanzibar.

Yanga wanaingia mechi ya Jumapili wakiwa roho juu wakijivunia kuwalemea watanio wao Simba, katika mechi zote sita za Ligi Kuu za hivi punde.

Ushindi pekee wa Wekundu wa Msimbazi Simba ni ule wa Kombe la Muungano wa bao moja kwa bila Jumatano wiki iliyopita.

Wekundu wa Msimbazi Simba, watahitaji ushindi ili kukata uongozi wa Yanga hadi alama 2, wakati Yanga maarufu kama Jangwani Boys, wakilenga ushindi ili kutanua uongozi wao hadi 8, kileleni pa jedwali.

Yanga wanashikili kukutu uongozi wa Ligi hiyo kwa pointi 47, wakifuatwa na Simba kwa alama 42,alama 5 zaidi ya Azam United FC, wanaokalia nafasi ya tatu.

Refa wa kati atakuwa Hamza El Faruq akisaidiwa na msaidizi wa kwanza Lahsene Azkawi,na Hamza El Nasri, atakayekuwa msaidizi wa pili huku Mostafa Kchaaf, akiwa afisa wa nne.

Share This Article