Timu 7 za Afrika miongoni mwa 48 zilizofuzu mashindano ya Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu saba za Afrika ni miongoni 48, zilizowahi tiketi za mashindano ya Riadha Ulimwenguni mwaka ujao jijini Beijing,Uchina.

Timu hizo zilifuzu katika raundi ya kwanza ya mihujo ya mbio za dunia za kupokezana kijiti mjini Gaberone, Botswana, siku ya Jumamosi.

Kenya ilifuzu katika mbio za mita 400 kwa wanariadha wanne mseto, baada ya kumaliza ya pili katika mchujo wa tatu.

Kando na Kenya timu nyingine zilizojikatia tiketi katika mbio hizo ni; Australia, Uingereza,Italia, Jamaica, Poland,Uhispania na Marekani.

Nafasi zilizosalia zitawaniwa Jumapili ambapo timu nne ,zikiwa mbili bora kila mchujo pia zitajikatia tiketi.

Wanawake 4x100m: Canada, China, Germany, Italy, Jamaica, Poland, Portugal, Spain

Wanaume 4x100m: Australia, Botswana, Canada, Germany, Great Britain & NI, Netherlands, South Africa, United States

Wanawake 4x400m: Canada, Czechia, Germany, Great Britain & NI, Italy, Netherlands, Norway, Spain

Wanaume 4x400m: Australia, Belgium, Botswana, Netherlands, Portugal, Qatar, South Africa, Zimbabwe

Mixed 4x100m: Canada, Germany, Great Britain & NI, Jamaica, Netherlands, Nigeria, Spain, United States

Mixed 4x400m: Australia, Great Britain & NI, Italy, Jamaica, Kenya, Poland, Spain, United States

Timu hizo zitashiriki mashindano ya Dunia ya mwaka ujao mjini Beijing,Uchina.

Share This Article