Ahly waikomoa Zamalek katika dabi ya Cairo

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara 45 wa Ligi Kuu nchini Misri Al Ahly, walifufua matumaini ya kufuzu kwa ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao baada ya kuwatitiga watani wa jadi Zamalek, mabao 3-0 katika dabi ya Cairo, iliyopigwa Ijumaa usiku jijini Cairo.

Ilikuwa mara ya tatu kwa Ahly kuwalemea Zamalek, msimu huu baada ya kuwashinda 2-0, katika duru ya kwanza ya Ligi Septemba mwaka jana na kuwalaza tena 2-1, Novemba mwaka jana katika fainali ya kombe la Super.

Zikisalia mechi mbili msimu ukamilike Pyramids, na Zamalek, wanaongoza jedwali kwa pointi 50, tatu zaidi ya Ahly, walio wa tatu.

Ahly wanahitaji kushinda mechi zilizosalia dhidib ya Enppi na Al Masry ili kuwa katika nafasi ya kufuzu kwa ligi ya mabingwa Afrika mwaka ujao.

Share This Article