Vlabu vya Barcelona na Liverpool, vitachuana katika mechi ya kirafiki inayotarajiwa kuchezwa jijini Nairobi Agosti nane, mwaka huu.
Timu hizo mbili zimeratibu mazoezi yao ya kabla ya msimu nchini Kenya, mwezi Agosti.
Itakuwa mara ya kwanza kwa Barca na Liverpool, kuzuru humu nchini.
Barca na Liverpool, walichuana kwa mara ya mwisho katika Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019, uwanjani Anfield, wenyeji Liverpool wakiinyuka Barca mabao 4-0.