Wanasiasa wahimizwa kusitisha kampeni za mapema

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya wafanyakazi Francis Atwoli.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafayakazi nchini Kenya Francis Atwoli, ametoa wito kwa wanasiasa kusitisha kampeni za mapema na badala yake kuwahudumia wakenya.

Akizungumza leo Ijumaa wakati wa maadhimisho ya 61 ya Leba Dei katika kaunti ya Vihiga, Atwoli alisema wafanyakazi wanasikitishwa sana na mikutano ya kisiasa kote nchini Kenya, kana kwamba Uchaguzi Mkuu unaandaliwa juma lijalo.

Katibu huyo aliitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, kuchukua hatua na kusitisha siasa za mapema, akiwahimiza wakenya kusubiri kalenda ya uchaguzi itakayotolewa na IEBC.

“Lazima tusitishe siasa za mapema na uchochezi. Mheshimiwa Rais ikiwa uchaguzi utaandaliwa na mshindi achaguliwe kwa njia ya haki, mazingira haya ya kisiasa yatasababisha matatizo hapa nchini,”  alisema Atwoli.

Maadhimisho ya mwaka huu yameandaliwa kwa mara ya kwanza nje ya Jiji Kuu Nairobi, huku Vihiga ikiwa kaunti ya kwanza kuwa mwenyeji wa sherehe hizo.

Share This Article