Mwili wa Spack wazikwa mkoani Tanga, Tanzania

Aliaga dunia, Aprili 27, 2026 ambapo alikutwa nyumbani kwake akiwa amefariki,

Marion Bosire
1 Min Read

Mwili wa marehemu mwanamuziki wa Bongo Fleva Selemani Ramadhan Mvamba maarufu kama Spack umezikwa leo Aprili 29, 2026 mkoani Tanga, nchini Tanzania.

Kakake Spack kwa jina Said alisema awali kwamba familia aliafikia uamuzi wa kumpumzisha huko Tanga, hali iliyolazimu usafirishaji wa mwili wakekutoka Dar es Salaam jana jioni.

Said alielezea pia kwamba Spack alifikwa na umauti akiwa ameketi kwenye kiti akitizama runinga, ambapo Watoto na Dada wa kazi walimamsha lakini hakuamka.

Spack alichapisha pia ujumbe tatanishi kwenye status yake ya WhatsApp saa 6 usiku kabla ya kufikwa na umauti akisema, “Hii ni Limited Edition na mission kabla ya kudanja.”

Mwanamuziki huyo ambaye amekuwepo kwenye tasnia ya muziki tangu mwanzo wa miaka ya 2000 aliaga dunia, Aprili 27, 2026 ambapo alikutwa nyumbani kwake akiwa amefariki, huku chanzo cha kifo chake kikichunguzwa.

Rafiki yake wa karibu, ambaye pia ni mwanamuziki Tunda Man, ambaye waliwahi kufanya kazi pamoja kwa ukaribu alieleza kuwa Spack hakuwa akionyesha dalili zozote za kuwa na changamoto ya kiafya.

Tunda Man alisema pia kwamba Spack alikuwa akiendelea kufanya maonyesho yake ya Chaka to Chaka ambapo alibainisha kuwa hivi karibuni walikuwa wakijadiliana namna ya kukamilisha kazi zao za muziki pindi watakapopata nafasi.

Share This Article