Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amewasili Jijini Accra, Ghana, kuhudhuria mkutano wa ngazi za juu wa Tana kuhusu usalama barani Afrika.
Mkutano huo unawaleta pamoja viongozi na wadau kutoka Afrika, kujadili suluhu za kiafrika kuhusu upatikanaji amani, uongozi na changamoto za kiusalama za kanda.
Alipowasili, Uhuru alilakiwa na balozi wa Kenya nchini Ghana Kanalai mstaafu Shem Ishmailidza Amadi.
Kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa X, Rais huyo mstaafu anahudhuria mkutano huo kama mwanachama wa Bodi ya Mkutano wa Tana, wadhifa aliouchukua mwaka 2024.
Uteuzi wake unamweka miongoni mwa kundi la Marais wa zamani wa Afrika wanaotoa uongozi wa kimkakati katika taasisi hiyo.
Jukumu la Kenyatta katika mkutano huo linatokana na juhudi zake za kutafuta amani barani Afrika, ambapo amehudumu kama mjumbe na mpatanishi kwenye Umoja wa Afrika.