Rais Ruto ampongeza Sawe kwa kuvunja rekodi ya Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais wa Kenya William Ruto.

Rais William Ruto amempongeza Mkenya Sebastian Sawe baada yake kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za marathon siku ya Jumapili.

Ruto ametaja ushindi huo wa Sawe katika London Marathon akiutaja kuwa hatua ya ujasiri na kudhihirisha Kenya kuwa taifa linalotoa miamba katika tasnia ya riadha.

Sawe alitwaa ushindi na kuvunja rekodi kwa muda wa saa 1:59:30, akivunja rekodi ya awali ya dunia ya saa 2:00:35 iliyowekwa na marehemu Kelvin Kiptum katika mbio za marathoni za Chicago mwaka 2023.

Aidha,Rais aliwapongeza Hellen Obiri na Joyceline Jepkosgei kwa kumaliza wa pili na wa tatu mtawalia katika mbio za wanawake.

Share This Article