Mashemeji kupimana ubabe leo katika Derby ya 99

Dismas Otuke
1 Min Read

Derby ya 99 ya Mashemeji kati ya mahasimu wa jadi  AFC Leopards  na Gor Mahia itasakatwa leo  Jumapili Aprili 26, katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Mchuano huo utang’oa nanga saa tisa alasiri.

Vinara wa ligi Gor,  watalenga kuepuka kushindwa derby ya pili msimu huu, baada ya Ingwe kushinda mkondo wa kwanza goli moja kwa bila Disemba mwaka jana.

Mchuano huo utabaini uwezo wa aidha Gor au Leopards kushinda taji la ligi kuu ,Kogalo wakiwa kileleni kwa alama 58, tatu zaidi ya  watani wao walio katika nafasi ya pili zikisalia mechi sita msimu ukamilike.

Katika mechi 98 za awali kila timu imeshinda mechi 34 na 29 kumalizikia sare.

Tiketi za mechi hiyo zinauzwa kwa shilingi 300,500,1,000 na 2,000.

Share This Article