Mamlaka ya usimamizi wa vyuo vya kiufundi nchini -TTVETA, imekipokonya leseni chuo cha mafunzo ya usimamizi nchini (KIM), baada ya kukiuka viwango vya ubora vilivyowekwa.
TTVETA imetangaza kufunga kwa mabewa yote ya chuo hicho humu nchini huku ikifutilia mbali vyeti vya masomo vya stashahada na shahada vilivyotolewa na chuo hicho kuanzia mwaka 2018 hadi leo.
Chuo cha KIM kimeadhibiwa kwa kukiuka sheria za 17(3) kutoa mafunzo kwa kozi ambazo hazijaidhinishwa kwa wanafunzi.
TTVETA imetahadhirisha umma dhidi ya kujihusisha na chuo hicho.