Msemaji wa serikali Isaac Mwaura, leo Alhamisi ameteta vikali mpango wa serikali kwa serikali almaarufu (G2G) wa ununuzi mafuta, akisema umeleta udhabiti katika usambazaji wa mafuta hapa nchini.
Katika mkutano na wanahabari kuhusu bei mpya za mafuta hapa nchini,Mwaura alisisitiza kuwa mkakati huo wa G2G umesababisha usambazaji shwari wa mafuta katika muda wa miaka mitatu iliyopita.
Hatibu huyo wa serikali alipongeza mpango huo akisema umefanikisha kuondoa uhaba wa bidhaa hiyo na udanganyifu uliohusishwa na mfumo uliokuwepo awali.
“Uhaba wa mafuta ulioshuhudiwa hapo awali uliotokana na mfumo wa ununuzi wa papo hapo ambao pia ulisababisha sarafu ya dola kuhodhiwa, sasa umetatuliwa na kuwezesha kupatikana kwa dola hatua inayofanikisha biashara za kigeni,” alisema Mwaura.
Aliwapuuzilia mbali wanaopinga mpango wa G2G akiwataja wanaoongozwa kisiasa, akisema wamekosa kuoma mafanikio yanayoshuhudiwa katika usambazaji wa mafuta na udhabiti wa shilingi ya kenya.
Aidha alishikilia kuwa mfumo wa G2G umeimarisha ubadilishanaji wa fedha za kigeni, na kuleta mipangilio bora kwa usambazaji wa mafuta wa Kenya.