Raia wa China afungwa mwaka mmoja gerezani kwa kusafirisha mchwa

Jaji Irene Gichobi wa  Mahakama ya uwanja wa JKIA, alisema raia huyo wa China hakuwa mkweli, na alikosa huruma.

Tom Mathinji
1 Min Read
Raia wa China ahukumiwa miaka mmoja gerezani kwa kosa la kusafirisha mchwa.

Raia wa China, Zhang Kequn, amehukumiwa mwaka mmoja gerezani au faini ya shilingi milioni moja, baada ya kupatikana na kosa la kujaribu kusafirisha mchwa kutoka Kenya.

Zhang alikamatwa mwezi mmoja uliopita katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), akiwa na zaidi ya mchwa 2,000 kwenye mkoba wake.

Jaji Irene Gichobi wa  Mahakama ya uwanja wa JKIA, alisema raia huyo wa China hakuwa mkweli, na alikosa huruma.

Mamlaka za Kenya zimeonya watu dhidi ya kuwakamata mchwa hao, ambao uhitaji wake umeongezeka bara Ulaya na Asia na huuzwa takriban $ 220 kila mmoja.

Shirika la Huduma kwa Wanyamapori KWS, liliwapongeza wale wote waliohusika na kukamakwa na kushtakiwa kwa mshukiwa huyo, huku likitoa wito kwa wakenya kuwaripoti wanaotekeleza biashara haramu ya wanyamapori.

Share This Article