Waimbaji wa nyimbo za injili Ben Serugo and Mbanza Chance maarufu kama Ben & Chance wanapanga kuandaa tamasha jijini Brussels nchini Ubelgiji Jumapili, Aprili 18, 2026.
Hatua hii inajiri baada ya wawili hao kuandaa tamasha sawia nyumbani jijini Kigali katika ukumbi wa BK Aprili 5, 2026.
Wanandoa hao walipitia Ufaransa Jumanne Aprili 14, 2026 kabla ya kutua katika jiji kuu la Ubelgiji kwa ajili ya maandalizi ya tamasha hilo la Jumapili.
Tamasha hilo la Brussels lilistahili kufanyika tarehe 5 mwezi huu wa Aprili lakini mipango ikabadilika baadaye kufuatia majadiliano na mwandaaji.
Matamasha ambayo Ben & Chance wanaandaa katika siku za hivi karibuni ndani na nje ya Rwanda, ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 15 katika uimbaji kama wanandoa.
Safari yao ilianza mwaka 2011 wakati wote wawili walikuwa wanachama wa kwaya moja maarufu kwa nyimbo za kuabudu ya Alarm Ministries.
Baada ya hapo waliondoka kwenye kwaya hiyo na kuamua kuimba wakiwa wawili, na wamekua sana kiasi kwamba wao ni kati ya makundi pendwa ya waimbaji wawili wawili nchini Rwanda kwa sasa.