Harambee Starlets kufungua FIFA Series dhidi ya India leo

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya wanawake ya soka,Harambee Starlets itashuka katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo leo Jumamosi kuanzia saa kumi na moja jioni kwa nusu fainali ya mechi za kirafiki almaarufu FIFA series.

Kenya watatumia mchuano huo kujipiga msasa kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON), kuanzia Julai mwaka huu nchini Morocco.

Mshindi wa mechi ya Kenya na India atamenyana  na mshindi wa nusu fainali ya pili ya kwanza kati ya Australia na Malawi.

Ni mara ya kwanza kwa Kenya kuandaa mechi hizo za FIFA.

 

 

Share This Article