Kenya yaimarisha vita dhidi ya homa ya Dengue

Tom Mathinji
1 Min Read
Mary Muthoni - Katibu katika Wizara ya Afya

Kenya inaimarisha juhudi za kukabiliana na homa ya Dengue pamoja na hatari zingine za kiafya chini ya mpango wa ‘Afya Moja’ unaotekelezwa na wizara ya Afya.

Akizungumza kwenye mkutano kuhusu homa ya Dengue nchini Ufaransa, Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni, alisema  kwenye mkutano huo, Kenya ilipigia debe ushirkiano wa kimataifa kuimarisha uwezo wa kutambua, kutibu na utoaji chanjo wa homa hiyo.

Kulingana na Muthoni, hatua hizo zinatekelezwa kwa kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tahadhari ya mapema, kuongeza udhibiti wa wadudu katika jamii, kupanua uwezo wa maabara kupitia shirika la KEMRI, na kuimarisha uratibu wa sekta mbalimbali.

Katibu huyo alibainisha kuwa uhamasishaji wa kiafya kuhusu magonjwa hayo unatekelezwa na wahudumu wa afya ya jamii ambao wako katika maeneo tofauti ya nchi.

Homa ya ‘Dengue’ inatokana na virusi vya ‘Dengue’ ambavyo kwa kiwango kikubwa husambazwa kwa binadamu kupitia mbu walioambukizwa.

Mkutano huo uliwaleta pamoja Mawaziri wa Afya, wanasayansi, waratibu sera na washirika katika sekta ya afya.

Share This Article