Waziri Duale:Zaidi ya hospitali 1,000 za kibinafsi  zimefungwa kwa kujaribu kuiba hela za SHA

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri wa Afya Aden Duale ,amesema kuwa zaidi ya hospitali za kibinafsi 1,000, nchini zimefungwa baada ya kujaribu kutapeli pesa za mamlaka ya Afya ya umma SHA.

Akizungumza Jumamosi Waziri Duale  amefichua kuwa baadhi ya hospitali hizo zimo katika kaunti za  Homa Bay,Bungoma,Mandera,Wajir na Kisii akisisitiza kuwa hsopitali zaidi ya 10 zimenaswa na kufungwa mwezi Machi pekee.

Aidha hospitali nyingine 250 zinachungwa na maafisa wa DCI,30 zikiwa zimefunguliwa mashataka huku nyingine 18 zikifikishwa kortini.

Alisema haya Jumamosi alipohudhuria  mahafala ya kufuzu kwa wasichana waliokamilisha masomo ya dini ya Kiislamu katika kituo cha Hawa Kosar  ambapo wasichjana 25 walihitimu.

 

 

Share This Article