Harambee Starlets kuwania tuzo ya SOYA

Dismas Otuke
1 Min Read
Timu ya taifa ya soka ya akina dada Harambee starlets.

Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets imeteuliwa kuwania tuzo ya timu bora katika makala ya 22 ya tuzo za Soya zitakazoandaliwa  katika bustani ya Uhuru tarehe 10 mwezi huu.

Starlets wameteuliwa baada ya kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON), zinazotarajiwa kaundaliwa mwaka huu nchini Morocco.

Itakuwa mara ya kwanza kwa Starlets kushiriki kipute cha WAFCON tangu mwaka 2016.

Aidha ,Starlets walimaliza katika anfasi ya pili wakati wa michuano ya CECAFA, iliyoandaliwa nchini Tanzania.

Timu nyingine zinazowania tuzo hiyo ni timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ya Voliboli , timu ya taifa ya raga ya wanawake na timu za mpira wa kikapu ya KPA na ile ya magongo.

Tuzo ya timu za wanaume inawaniwa na mabingwa wa Kenya Cup Kabras Sugar RFC,

Nairobi City Thunder,Nairobi United,timu ya Voliboli ya  Junior Wafalme Stars na Harambee Stars.

Share This Article