Seneta wa Siaya Oburu Odinga amekabidhiwa rasmi uongozi wa chama hicho kwenye mkutano maalum (SDC), ulioandaliwa Ijumaa katika uwanja wa Jamhuri kaunti ya Nairobi.
Mkutano huo, aidha, uliwaidhinisha Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir na mwenzake wa Kisii Simba Arati kuwa manaibu wenyeviti.
Wajumbe hata hivyo walimfurusha Gavana wa Vihiga Godfrey Osotsi kutoka kwa wadhifa aliokuwa akishikilia wa naibu mwenyekiti katika hali tatanishi huku wakikataa kupendekeza jina lake.
Yamkini inafuatia na hali ya Osotsi kuonekana akijihusisha na kundi pinzani la Linda Mwananchi, linaloongozwa na Katibu Mkuu Edwin Sifuna.