Mshukiwa wa ulaghai wa dhahabu bandia afikishwa mahakamani

Martin Mwanje
1 Min Read

Mshukiwa wa ulaghai wa dhahabu bandia ya dola za Marekani 600,000 amefikishwa katika mahakama ya Milimani kujibu mashtaka. 

Ulaghai huo ulimlenga raia wa Australia.

Duncan Okaka Okonji alikamatwa Machi 24, 2026 na kuwasilishwa mahakamani jana Alhamisi.

Mkenya huyo alishtakiwa kwa njama ya ulaghai kinyume cha sehemu ya 317  ya Kanuni ya Adhabu.

Alikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 au dhamana mbadala ya shilingi milioni moja pesa taslimu.

Kesi hiyo imepangwa kutajwa Aprili 7, 2026 katika mahakama ya Milimani.

Share This Article