Kenya Airways yanakili hasara ya shilingi bilioni 17

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwenyekiti wa Shirika la Ndege la Kenya Airways Kiprono Kittony.

Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ), limetangaza hasara ya shilingi 17.2, katika kipindi kilichokamilika mwezi Disemba mwaka 2025.

KQ ilisema kuwa licha ya ongezeko la wateja, shirika hilo halikuwa na idadi ya kutosha ya ndege hatua iliyosababisha kushuka kwa mapato ya wateja kwa asilimia 18, huku mapato ya uchukuzi wa mizigo ikishuka kwa asilimia nane.

“ Tulikuwa na wateja waliotaka kusafiri nasi, lakini hatukuwa na ndege za kutosha kuwasafirisha,” alisema mwenyekiti wa shirika hilo Kiprono Kittony.

Kutokana na changamoto za operesheni zake, shirika hilo lilisema mapato yalipungua kwa asilimia 14 baada ya kupata shilingi bilioni 161.5, ikilinganishwa na shilingi bilioni 188.5 ilizokusanya mwaka uliotangulia.

Wakati wa kipindi hicho, shirika hilo lilitekeleza asilimia 80 ya operesheni zake kutokana na kuharibika kwa baadhi ya ndege zake.

Hata hivyo, ndege zilizoharibika zilipunguza gharama za operesheni hadi shilingi bilioni 179.4 kutoka shilingi bilioni 183 mwaka uliotangulia.

Share This Article