Rais William Ruto siku ya Jumatatu amefungua hospitali mpya ya Level 3 ya Piny Owacho katika eneo bunge la Uriri, kaunti ya Migori.
Akizungumza baada ya kuifungua hospitali hiyo, Rais aliahidi kuhakikisha kuwa ina vifaa vya maabara vyote na vya kutosha na madaktari wa kutosha ili kuhudumia jamii vyema.
Aidha, aliongeza kuwa serikali yake imewekeza shilingi bilioni 2.4 kuimarisha vituo vya afya katika kaunti ya Migori katika juhudi za kutoa huduma bora za afya ambayo ni nguzo kuu ya serikali yake.