Kocha Cheche ataja kikosi kwa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Namibia mwezi ujao

Dismas Otuke
2 Min Read

Kocha wat imu ya taifa ya Kenya kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 ukipenda Junior Starlets Mildred Checheametaja kikosi kitakachocheza na Namibia mwezi ujao kwa mchujo wa kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.

Cheche amewajumuisha wachezaji wenye tajriba na limbukeni kwa mechi hiyo ya raundi ya ambayo mkondo wa kwanza utaandaliwa nchini Namibia Aprili 12,kabla ya marudio kufanyika  Kenya siku sita baadaye.

Mshindi wa kati ya Namibia na Kenya atachuana na atakayeshinda baina ya Uganda na Zimbabwe kwenye raundi ya pili mwezi Mei.

Timu 15 bora baada ya raundi tatu za mchujo zitajiunga na wenyeji Morocco kwa fainali za Kombe la Dunia kati ya Oktoba 17 na Novemba 7 mwaka huu.

Kikosi hicho cha awali kinawajumuisha;

Makipa

Mitshel Ng’ono (Wiyeta girls), Vallary Achieng (Nyakach girls), Martha Mitchelle (Nasokol girls), Roseline Achondo(Tumaini Secondary)

Mabeki

Pauline Namisi (Desert scorpions), Faith Boke (Butere girls), Idah Matara (Nyakach girls), Ruth Barasa (Wiyeta girls), Daisy Adongo (Gideon starlets), Sheila Atieno (Nyakach girls), Grace Mumo (Madira girls), Rose Nangila (Amus college), Brenda Otieno (Kobala secondary)

Kiungo cha kati

Bevarline Awuor (Mathare United), Bakari Mwanakombo (Kombani secondary), Brenda Awuor(Madira girls), Gaudancia Maloba (Lwak girls), ⁠Noelina Akuku (Butere girls), Lindi Weey Atieno (Madira girls), Beryl Awuor (Nyakach girls), Fleviah Khatenje (St. Joseph girls Kitale)

Washambulizi

Brenda Achieng (Kakamega hill), Patience Waithera (St. Joseph Murang’a), Khadija Furaha (Kobala Secondary), Emily Adhiambo (Nyakach girls), Tabitha Wambui (Madira girls), ⁠Ivy Atieno (St. Joseph girls kitale), ⁠Lilyann Adhiambo (Kibera soccer women), Melvin Vugutsa (Annet Mixed secondary), Elizabeth Alizeba (Oding JSS)

Share This Article