Ruto aendeleza sakasaka za kura Nyanza kwa kufungua miradi ya maendeleo

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto aliendeleza kampeni zake za kuwashawishi wapiga kura wa eneo la Nyanza kumuunga mkono kwa muhula wa pili Ikuluni katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Siku ya Jumapili, Ruto alihudhuria ibada katika shule ya upili ya Agoro Sare eneo bunge la Kasipul, kaunti ya Homa Bay.

Akiwa katika kaunti ya Homa Bay, Ruto alifungua ujenzi wa barabara ya Ring katika kisiwa cha  Rusinga.

Barabara hiyo ya umbali wa kilomita 298 itagharimu serikali shilingi bilioni 17.

Baadaye, Rais pia alikagua barabara ya Karabok-Adiedo, yenye umbali wa kilomita 7.34 kwa gharama ya shilingi milioni 925, katika eneo bunge la Karachuonyo.

Ruto amekita kambi katika eneo la Nyanza tangu wiki jana alipofungua ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Kisumu hadi Malaba siku ya Jumamosi pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Share This Article