Waislamu nchini washerehekea sikukuu ya Idd

Sikukuu ya Idd Ul Fitr huashiria kukamilika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waislamu kote nchini Kenya wamemiminika misikitini mapema leo Ijumaa kuadhimisha sikukuu ya Idd Ul Fitr, inayoashiria kukamilika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Misikiti mingi katika kaunti ya Nairobi ilijaa waumini waliopiga dua kabla ya kaunza shamrashamra za Idd.

Waziri wa Afya Aden Duale alijumuika na waumini katika msikiti wa Sir Ali kwa maombi na kuutaka upinzani kuzingatia siasa za ajenda zinazowahusu wananchi.

Duale pia ameyasuta mashirika ya kijamii kwa kutowakomesha viongozi wa upinzani wakati wamekuwa wakimtusi Rais, badala yake yanamkosoa Rais wakati anapoujibu upinzani.

Naye Waziri wa Michezo Salim Mvurya alijumuika na waumini katika eneo la Moyeni, eneo bunge la Kinango, kaunti ya Kwale, kwa maombi ya Idd.

Tunawatakia Waislamu wote Eid Mubarak.

Share This Article