Chad imesema italipiza kisasi baada ya Sudan kutumia ndege zisizo na rubani kufanya shambulizi na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby, akiwa amevalia sare za kijeshi aliitisha mkutano wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa, huku akiagiza jeshi la nchi yake kulipiza kisasi dhidi ya shambulizi hilo la Sudan.
Wakati huo huo, Rais huyo aliagiza kufungwa kwa mpaka kati ya nchin hiyo na Sudan, akisema kuwa serikali yake imeimarisha usalama kwenye mipaka.
Mpaka wa Chad na Sudan, ambao una urefu wa takriban kilomita 1,400, uko kwenye jangwa na umetajwa kuwa hatari na mgumu kudhibiti.
Kundi la wapiganaji la Rapid Support Forces (RSF), lilikanusha kuhusika kwenye mashambulizi hayo na badalka yake kuelekeza kidole cha lawama kwa jeshi la Sudan.