Zendaya akosa kufichua iwapo alifunga ndoa na Tom Holland

Alikuwa katika kipindi cha Jimmy Kimmel Live kutangaza filamu yake mpya wakati Jimmy aliibua suala hilo la ndoa.

Marion Bosire
1 Min Read

Zendaya Maree Stoermer Coleman mwanamuziki na mwigizaji wa Marekani ambaye wengi wanamfahamu kwa jina lake la kwanza ‘Zendaya’ ameendeleza utata kuhusu iwapo alifunga ndoa.

Nyota huyo alikuwa mgeni katika kipindi cha Jimmy Kimmel Live kutangaza filamu yake mpya iitwayo “The Drama” wakati Jimmy aliibua suala hilo la ndoa.

Kumekuwa na uvumi mitandaoni kwamba Zendaya alifunga ndoa na Tom Holland ingawa wawili hao hawajatangaza hilo.

Jimmy alitaja taarifa ambazo zimekuwa zikienea kuhusu ndoa hiyo kama njia ya kumchochea Zendaya kufunguka na mwanamuziki huyo akasema hajaona taarifa hizo.

Walizungumza pia kuhusu picha za filamu ya The Drama, zilizobadilishwa kwa kutumia akili unde ambapo Zendaya na Robert Pattinson, waliigiza wakifunga ndoa na uso wa Pattinson ukabadilishwa na ule wa Tom Holland.

Zendaya alisema kwamba wengi wamehadaika na picha hizo wakiwemo watu wa familia na marafiki wa karibu, ambao walikasirika kwa kutoalikwa harusini. Alithibitisha kwamba picha hizo sio za kweli.

Mwanamuziki huyo ambaye pia ni mwigizaji alimaliza mahojiano bila kukana au kukubali kwamba amefunga ndoa na Tom Holland.

Law Roach ambaye ni msanifu mitindo wa Zendaya, ndiye alianzisha uvumi kuhusu ndoa ya Zendaya na Holland pale aliposema kwenye mahojiano kwamba kila mmoja alikosa harusi ya wawili hao.

Share This Article