Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imeanzisha msako dhidi ya mshukiwa anayedaiwa kutekeleza uhalifu wa ubakaji na mauaji.
Kulingana na idara hiyo, mshukiwa huyo anaaminika kumbaka na kisha kumuua mwanamke mwenye umri wa miaka 28 Machi 12 mwaka huu.
Mshukiwa huyo ambaye alitoroka, anatoka katika kijiji cha Ngushui, taarafa ya Murinduko, eneo bunge la Mwea, kaunti ya Kirinyaga.
Kwenye ukurasa wa X, DCI imesema mshukiwa huyo ni hatari na anamiliki silaha.
“Yeyote aliye na habari kumhusu anapaswa kuripoti mara moja,” ilisema DCI kwenye ukurasa wa X.
Habari kumhusu mshukiwa zinaweza tolewa kupitia #FichuaKwaDCI, nambari za simu 0800 722 203 au mtandao wa WhatsApp kupitia 0709 570 000.